Ndugu wanajumuiya ya SUA,

Kutokana na mwenendo wa ugonjwa wa COVID-19 nchini menejimenti ya Hospitali inachukua tahadhari hatua kwa hatua. Lengo likiwa ni kupunguza/kuzuia  uwezekano wa kusambaa kwa ugonjwa huo iwapo utakuwepo katika maeneo yetu bila kuutarajia.
Hivyo basi kwa wagonjwa wote wanaohitaji huduma ya tiba katika Hospitali ya Chuo pia Wauguzaji au ndugu wanaokuja kusalimia wagonjwa, wanawajibika muda wote wawapo katika mazingira ya Hospitali kutimiza masharti yafuatayo:-
1.  Kuvaa barakoa ya aina yoyote
2. Kusafisha mikono kwa maji tiririka na sabuni au kitakasa mikono( sanitizer) waingiapo au kutoka katika mazingira ya Hospitali (huduma hiyo inapatikana  hospitali bure)
3. Wauguzaji , ndugu au jamaa wote wanaokuja kuwatembelea wagonjwa waliolazwa wanapaswa kuzingatia agizo la Wizara ya Afya linaloelekeza  awepo mtu mmoja tu kwa mgonjwa aliyelazwa kwa muda mfupi. Aidha hairuhusiwi  kuingia wadini kiholela au kwa kundi la watu wengi kwa wakati mmoja
3 users found this usefulWas this information useful?Yes